Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Derby ya Kariakoo dhidi ya watani wa jadi Yanga.
Wachezaji wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na wamejitahidi kuonyesha uwezo ili kulishawishi benchi la ufundi kuwapa nafasi.
Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake wamesimamia mazoezi hayo na wameridhishwa na viwango vya wachezaji.
Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunaiheshimu Yanga lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi.