Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili, Novemba 5.
Timu iliingia kambini Jumanne kujiandaa na mchezo huo mkubwa ambao unavuta hisia kali za mashabiki kote ndani na nje ya nchi.
Wachezaji wameshiriki mazoezi hayo kikamilifu na morali yao iko juu lengo likiwa ni kuhakikisha tunapata alama tatu.