Timu yarejea jijini Dar es Salaam

Kikosi chetu kimerejea salama jijini Dar es Salaam kutoka nchini Misri baada ya jana kucheza na Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa African Football League (AFL) uliomalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Baada ya kikosi kufika wachezaji wamepewa mapumziko na kesho watarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Ihefu FC.

Mchezo wetu dhidi ya Ihefu utapigwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Tutakuwa na siku mbili za kujiandaa na mchezo dhidi ya Ihefu lakini tunaamini maandalizi yetu yatatufanya kupata matokeo chanya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER