Mchezo wetu wa ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly kutoka Misri uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.
Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kawaida tulimiliki mpira kwa kiasi kikubwa huku Al Ahly wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.
Reda Salim aliwatanguliza Al Ahly kwa kuwafungia bao la kwanza dakika ya 45 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Amro Mohamed.
Kibu Denis alitupatia bao la kusawazisha kwa kichwa dakika ya 50 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Clatous.
Sadio Kanoute alitupatia bao la pili kwa kichwa cha mkizi dakika ya 59 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Saido Ntibazonkiza.
Bao hilo halikudumu kwani Mahmoud Kahraba aliisawazishia Al Ahly dakika mbili baadae baada ya walinzi wetu kuchelewa kuokoa mpira wa adhabu.
Baada ya kuruhusu bao hilo wachezaji walijitahidi kutafuta la ushindi lakini hata hivyo Al Ahly walikuwa imara katika kuzuia.
X1:Ally, Kapombe (Israel 75′), Zimbwe Jr, Che Malone, Henock, Ngoma, Chama (Bocco 85′), Mzamiru (Kanoute 45′), Ntibazonkiza, Miquissone (Baleke 45′), Kibu Denis (Onana 75′)
Walioonyeshwa kadi: Baleke 60′ Kanoute 73′
X1: ElShenawy, Moustaf, Yesser, Kahraba (Mohsen 78′) Tau, Slim (Attia 67′), Dieng, Afsha (El Shahat 67′), Hany,Eldebes, Kola
Walioonyeshwa kadi