Tumeondoka na alama zote Manungu

Tumefanikiwa kupata alama zote tatu katika mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuichapa Mtibwa Sugar mabao 4-2 katika mtanange uliopigwa Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro.

Jean Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya tano akimalizia mpira krosi uliopigwa kwa mguu wa kushoto na Kibu Denis kutoka upande wa kulia.

Essomba Onana alitupatia bao la pili dakika ya tisa kwa shuti la mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 kufuatia shuti la Baleke kuokolewa na mlinda mlango wa Mtibwa, Mohamed Makaka.

Mtibwa walipata bao la kwanza dakika ya 20 kupitia Matheo Anthony kwa shuti kali ndani ya 18 akimalizia pasi ya Juma Liuzio.

Dakika mbili baadae Matheo aliisawazishia Mtibwa baada ya kupokea pasi ndefu na kuwazidi ujanja walinzi wetu akitokea upande wa kushoto.

Kiungo Fabrice Ngoma alitupatia bao la tatu kwa kichwa dakika ya 44 kufuatia mpira mrefu wa krosi uliopigwa na Shomari Kapombe ambao ulimkuta Sadio Kanoute na baadae Baleke kabla ya kutua kwa mfungaji.

Clatous Chama alitupatia bao la nne dakika ya 80 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Luis Miquissone.

X1: Makaka, Kasami, Yassin, Mo. Kassim, Nasry, Nyangi, Hillary (Mkopi 86′), Chasambi (Tiote 88′), Nashon (Khamis 50′) Anthony, Liuzio (Karihe 63′)

Walioonyeshwa kadi: Nashoni 24′ Hillary 57′ Karihe 90+1

X1: Ally, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy (Kazi 86′), Che Malone, Kanoute (Mzamiru 45′), Chama, Ngoma, Baleke (Miquissone 63′), Kibu (Phiri 78′), Onana (Ntibazonkiza 45′)

Walioonyeshwa kadi: Baleke 63′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER