Tupo tayari kwa fainali Ngao ya Jamii

Leo saa moja usiku kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa CCM Mkwakwani kuikabili Yanga kwenye mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii.

Kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho jana jioni na wachezaji wapo tayari kwa mchezo ambao tunatarajia utakuwa mgumu.

Robertinho afunguka.

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa licha ya ugumu wa mechi utakaokuwepo lakini turakitahidi kucheza soka safi la kuvutia.

Robertinho amesema tutacheza kwa kushambulia na kuzuia kwa pamoja lengo likiwa ni kuhakikisha tunapata matokeo chanya yanayoambatana na soka safi.

“Ni mchezo muhimu wa Derby, mechi hii huwa haitabiliki, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kucheza vizuri na kushinda,” amesema Robertinho.

Chama atakuwepo.

Kiungo mshambuliaji, Clatous Chama atakuwepo kwenye mchezo wa leo baada ya kumaliza adhabu ya kukaa nje ya uwanja kwa michezo mitatu.

Israel atoa neno.

Mlinzi wa kulia, Israel Patrick amesema wachezaji wanajua umuhimu wa ushindi kwenye mchezo wa leo na wamejipanga kuhakikisha tunatwaa taji.

“Tunajua umuhimu wa ushindi kwenye mchezo leo, Wanasimba wanahitaji furaha na tupo tayari kuhakikisha tunawapatia,” amesema Israel.

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER