Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga fainali ya Ngao ya Jamii baada ya kuifunga Singida Fountain Gate kwa mikwaju ya penati 4-2 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Mkwakwani baada ya sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida.
Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini umakini kwenye eneo la mwisho ulikosekana.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuliandama lango la Singida huku Singida wakionekana kukaa nyuma na kufanya mashambulizi machache ya kushtukiza lakini safu yetu ya ulinzi ilikuwa imara.
Mlinzi wa kati Henock Inonga alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumizwa bega na mshambuliaji Medie Kagere.
Penati zetu zimefungwa na Luis Miquissone, Saido Ntibazonkiza, Mzamiru Yassin na Moses Phiri.
Kwa upande wa Singida penati zao zimefungwa na Tchakei na Duke Abuya huku Aziz Andambwile na Yusuph Kagoma walikosa.
Matokeo ya leo yanatufanya kukutana na watani wa jadi Yanga kàtika mchezo wa fainali utakaopigwa Jumapili.
X1: Kakolanya (30), Kijili (22), Gadiel (12), Carno (23), Mangalo (2) Kagoma (21), Abuya (30), Chukwu (11), Ambundo (7) (Andambwile 87′) Kazadi (17) (Kagere 67′) Tchakei (20)
Walioonyeshwa kadi: Chukwu 3′ Tchakei 46′ Beno 48′ Kijili 75, Kagoma 85′
X1: Ally (1), Kapombe (12), Zimbwe Jr (15), Che Malone (20), Inonga (29) (Kennedy 90+3) Kanoute (8) (Ngoma 45), Ntibazonkiza (10), Mzamiru (19), Baleke (4) (Bocco 45′), Kibu (38) (Phiri 59′), Onana (7) (Miquissone 71′)
Walioonyeshwa kadi: Onana 58′