Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Alhamisi katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.
Wachezaji wote wameshiriki mazoezi hayo na hakuna aliyepata maumivu ambayo yatamfanya kuukosa mchezo wa Alhamisi.
Baada ya mazoezi hayo kikosi kinajiandaa na safari ya Tanga kamili kwenda kushiriki michuano ya Ngao ya Jamii ambayo safari hii inashirikisha timu nne.