Wachezaji wapimwa uzito Uturuki

Ikiwa zimepita siku tatu tangu tuanze maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa mashindano 2023/24 leo asubuhi wachezaji wamepimwa uzito.

Sababu ya kupimwa uzito ni kutaka kuonyesha utimamu wao wa mwili ili kupangiwa vyakula ambavyo wanapaswa kutumia katika kipindi hiki cha maandalizi.

Baada ya vipimo hivyo vilivyofanyika asubuhi jioni wachezaji walifanya mazoezi magumu ya uwanjani ambapo walitakiwa kukimbia muda mwingi ili kujaza pumzi.

Kocha msaidizi, Ouanane Sellami amesema kwa mujibu wa programu iliyopo wachezaji wataendelea kuwa na mazoezi magumu kwakuwa ndivyo inavyotakiwa hasa mwanzoni mwa maandalizi ya msimu.

“Mazoezi tuliyofanya leo yalikuwa na umuhimu wa kuongeza utimamu wa kila mchezaji ndio maana tuliwaweka vifaa maalumu (GPS) kwenye vifua vyao ili kuona yupi amefika pale panapohitajika na nani anatakiwa kuongezewa au kupungiziwa ili wote kuwa sawa na kwenda kwenye mashindano.”

“Mwishoni mwa maandalizi haya tutapunguza ugumu wa mazoezi ikiwemo kucheza mechi za kirafiki ili kuona tunachowapatia wachezaji kwa wakati huu wamekifanyia kazi kwa kiasi gani,” Kocha Sellami.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER