Zimbwe Jr aongezwa miaka miwili

Mlinzi wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kubaki kikosini mpaka 2025.

Zimbwe Jr ambaye ni nahodha msaidizi wa timu amekuwa muhimili mkubwa katika eneo la ulinzi hivyo benchi la ufundi limeona huduma yake bado inahitajika.

Zimbwe Jr ni miongoni mwa wachezaji waliocheza mechi nyingi tangu ajiunge nasi kutoka Kagera Sugar mwaka 2015 kutokana na kuaminiwa na makocha mbalimbali waliowahi kukinoa kikosi chetu.

Malengo yetu ni kuhakikisha tunarejesha mataji yetu tuliyopoteza hivyo tunapaswa kubakisha wachezaji wetu wote bora.

Zimbwe Jr anakuwa mchezaji wa pili kuongezwa mkataba baada ya mlinzi wa kulia Shomari Kapombe kusaini nae miaka miwili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER