Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewathibitishia Wanasimba kuwa msimu ujao wa ligi hatutakuwa wanyonge tumejipanga kusuka kikosi imara kwa ajili ya kushinda mataji.
Try Again amesema tutasuka kikosi imara kwa ajili ya kuhakikisha tunashinda mataji baada ya kuyakosa kwa miaka miwili.
“Naomba niwahakikishie Wanasimba wote kuwa msimu ujao hatutakuwa wanyonge, tutakuwa imara kuliko ilivyokuwa awali.
“Tunajua kwa misimu miwili hatukuwa na furaha lakini msimu ujao tutakuwa bora kwakuwa tutasajili kikosi imara,” amesema Try Again.