Ntibazonkiza akabidhiwa tuzo yake ya Emirate Aluminium

Kiungo mshambuliaji, Said Ntibazonkiza amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Mei (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Ntibazonkiza amekabidhiwa tuzo hiyo baada ya kuwashinda walinzi Shomari Kapombe na Henock Inonga ambao alikuwa ameingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Ntibazonkiza amewashukuru wadhamini Emirate Aluminium Profile, wachezaji wenzake na mashabiki kwa kufanikisha kuibuka mshindi.

Ntibazonkiza amesema tuzo za Emirate zinaongeza hamasa kwa wachezaji na kujitoa kwa kila hali kuisaidia timu kupata matokeo chanya uwanjani.

“Nawapongeza Emirate Aluminium Profile kwa kuona umuhimu wa hii tuzo kwetu. Tuzo hii inaongeza chachu ya kila mtu kujituma kuipa timu mafanikio.

“Nalishukuru benchi la ufundi kwa kunipa nafasi, wachezaji wenzangu kunipa ushirikiano uwanjani pamoja na mashabiki kwa kunipigia kura, naomba tuendelee na utaratibu huu msimu ujao,” amesema Ntibazonkiza.

Ntibazonkiza amekabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER