Matola apata mualiko Ghana

Kocha Mkuu wa timu za vijana, Selemani Matola amepata mualiko wa kwenda Accra Ghana kushuhudia mashindano ya vijana chini ya umri wa 23 yatayofanyika nchini humo kuanzia June 20 hadi 24 mwaka huu.

Mashindano hayo yamendaliwa na Taasisi ya Gateway Tours & Sports inayojihusisha na kuandaa mashindano ya mpira wa miguu na matukio mbalimbali ya kimichezo.

Katika mashindano hayo Taasisi hiyo imealika makocha na maskauti kutoka maeneo mbalimbali duniani akiwemo Matola.

Taasisi Gateway Tours & Sports italipia waalikwa wote gharama za tiketi, malazi na Chakula kwa muda wote wa mashindano.

Mashindano haya yataambatana na mafunzo ya kutambua na kuendeleza vipaji kwa wachezaji vijana.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER