Baada ya mapumziko ya siku kadhaa timu imerejea mazoezini kujiandaa na mechi mbili zilizozalia za kukamilisha msimu wa Ligi Kuu 2022/23.
Mazoezi hayo yamefanyika katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena chini ya kocha mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ pamoja na wasaidizi wake.
Mchezo wetu unaofaata utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigiwa Juni 6, wakati wa mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Coastal Union Juni 9 na zote tutakuwa nyumbani.