Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah ‘Try Again’ amewaomba radhi wanachama, mashabiki na wapenzi kwa kushindwa kutwaa taji lolote ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo.
Try Again amesema kwenye mpira hali hii ni kawaida na hatupaswi kunyoosheana videole badala yake kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.
Try Again ametaja vitu vitatu vilivyochangia kukosa taji lolote msimu huu kuwa ni majeruhi kwa wachezaji wetu, nyota tuliowaongeza kuahindwa kuonyesha ubora pamoja na ugumu wa ligi.
“Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi nachukua nafasi hii kuwaomba radhi Wanasimba wote, hatukuwa na msimu mzuri sababu tumekosa mataji yote.
“Tumekuwa na changamoto ya majeruhi kikosini, wale tuliowaongeza pia wameshindwa kuonyesha ubora lakini ndio mpira tunajipanga kwa msimu mpya,” amesema Try Again.