Licha ya kushindwa kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mamia ya mashabiki wetu wamejitokeza Uwanja wa Ndege wa Kimaitaifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) kuwapongeza wachezaji kwa kazi kubwa walioifanya.
Baada ya mchezo huo mashabiki walionyesha kufurahia viwango vya wachezaji na jinsi walivyopambana hadi mwisho na ndio sababu ya kujitokeza kwa wingi JNIA kuja kuwalaki.
Kikosi kimewasili kutoka nchini Morocco baada ya kupoteza kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Mabingwa watetezi Wydad Casablanca huku wakiwabana vilivyo usiku wa kuamkia jana.
Kwa sasa tunaelekeza nguvu katika mechi zetu zilizosalia za Ligi Kuu ya NBC pamoja na mchezo wetu wa Nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Azam FC utakaopigwa Mei 6, Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.