Kikosi chetu leo saa 11 jioni kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili watani wetu wa jadi Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefanya mabadiliko ya wachezaji sita ukilinganisha na kikosi kilichocheza mechi ya mwisho dhidi ya Ihefu.
Mlinda mlango Ally Salim ambaye alionyesha kiwango bora katika mchezo uliopita dhidi ya Ihefu amepewa nafasi ya kuanza leo.
Kikosi Kamili kilivyopangwa
Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Erasto Nyoni (18), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Jean Baleke (4), Saido Ntibazonkiza (39), Kibu Denis (38).
Wachezaji wa Akiba:
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Nassor Kapama (35), Peter Banda (11), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10).