Preview: Mchezo wetu dhidi ya Yanga

Leo saa 11 jioni kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Yanga katika mchezo wa ‘Derby’ wa Ligi Kuu ya NBC.

Mchezo huu ni muhimu kwetu kupata ushindi kwakuwa unabainisha hatma yetu kama tuna nafasi ya kupigania ubingwa au la.

Ukiacha kupigania pointi tatu ili kupunguza tofauti ya alama dhidi ya wanaongoza lakini pia tunahitaji kushinda ili kuweka heshima baada ya kushindwa kupata ushindi dhidi yao tangu mwaka 2019.

Taarifa ya Kikosi.

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema tutaingia kwenye mchezo tukifahamu utakuwa mgumu na tutawaheshimu wapinzani wetu lakini tupo tayari kuwakabili.

Robertinho amesema tuna mwenendo mzuri wa kushinda na kucheza vizuri katika mechi zetu zilizopita hivyo tutaitumia kama morali kuhakikisha tunashinda leo.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi na kucheza vizuri, nawajua vizuri wapinzani wetu Yanga tunawaheshimu lakini tumejipanga. Mpira kwangu ni sanaa napenda wachezaji wacheze na kuwafurahisha mashabiki pia,” amesema Robertinho

Mchezo wa Mzunguko wa kwanza uliisha sare.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Oktoba 23 ulimalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Sisi tulikuwa wa kwanza kufunga bao kupitia kwa Augustine Okrah wakati wao walisawazisha kupitia kwa Stephen Aziz Ki.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER