Kuelekea Derby Jumapili tumekuja na ‘Mnyama Package’

Zikiwa zimesalia siku nne kabla ya kukutana na watani wetu wa jadi Yanga tumekuja na mfumo mpya wa tiketi kwa ajili ya Marafiki kutoka kwenye makundi mbalimbali itakayojulikana kama ‘Mnyama Package’ ambazo zitauzwa kwa watu kuanzia 20.

Mnayama Package itakuwa ni kwa ajili ya kundi au marafiki ambao wanaweza kuwa wanatoka katika eneo moja au hata makundi ya Whatsapp.

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema lengo la kuleta Mnyama Package ni kupunguza usumbufu wa kupata tiketi na kuwafanya marafiki kukaa sehemu moja.

“Tiketi hizi za Mnayama Package zitakuwa zinauzwa hapa ofisini na zitakuwa kwa ajili makundi yote iwe VIP A, B, C Machungwa na mzunguko lengo likiwa ni kuondoa usumbufu na kuwafanya marafiki kukaa pamoja,” amesema Kajula.

Pia kutakuwa na Executive Tiketi kwa ajili ya Taasisi, Makampuni na Mashirika ambazo wafanyakazi wetu watazipeleka hadi ofisi za wahusika na gharama yake itakuwa Sh. 40,000.

Watakao nunua tiketi za Executive watapewa kibali cha kuingia na magari yao pamoja na vinjwaji laini.

Kama kawaida Tiketi za Platinum zitakuwepo kwa bei ya Sh. 150,000 ambapo wataonunua watasindikizwa na king’ora kutoka Serena Hotel hadi uwanjani na kurudi, watapata vinjwaji laini na vigumu pamoja na T-shirt Maalum kwa ajili ya mechi ya Derby.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER