Chama akabidhiwa tuzo yake ya Emirate

Kiungo mshambuliaji, Clatous Chama amekabidhiwa tuzo yake mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

Katika mwezi Machi, Chama amecheza mechi nne sawa na dakika 273 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa jingine moja.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Chama amewashukuru wachezaji wenzake, mashabiki na familia kwa mchango mkubwa mpaka kufikia hatua hiyo.

“Nawashukuru mashabiki wachezaji na familia yangu wamekuwa msaada mkubwa mpaka kufanikiwa kupata tuzo hii.

“Hii ni mara ya tatu kwangu kuchukua tuzo hii msimu huu, imekuwa chachu kubwa ikiongozwa na familia yangu, mashabiki na wachezaji wenzangu.”

“Kwa niaba ya wachezaji nawashukuru Emirate Aluminium kwa kudhamini tuzo hii anaamini watazidi kuwepo nasi kwakuwa tunawahitaji kwa ajili ya kuongeza hamasa,” amesema Chama.

Chama amekabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo na wadhamini Emirate Aluminium Profile kama sehemu ya zawadi ya ushindi huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER