Kikosi chetu leo kimeanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa maruadiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca ambao utakuwa wa mwisho wa hatua ya makundi.
Mchezo huo utapigwa katika Jiji la Casablanca, Machi 31 saa nne usiku kwa saa za Morocco ambapo hapa nyumbani itakuwa saa saba usiku, Aprili Mosi.
Wachezaji wote ambao hawapo kwenye majukumu ya timu za taifa wameshiriki mazoezi hayo chini ya kocha mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na wasaidizi wake.
Nyota waliokuwa kwenye timu za taifa nao wataungana na wenzao mara tu watakapomaliza majukumu yao.