Manula Mchezaji bora wa Mwaka BMT

Mlinda mlango, Aishi Manula amechaguliwa mchezaji bora wa mwaka katika hafla ya tuzo zinazotolewa na Baraza la Michezo Tanzania (BMT).

Manula amewapiku walinzi Mohamed Hussein na Shomari Kapombe alioingia ingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho ambao wote wanatoka kwenye kikosi chetu.

Tuzo hiyo imepokelewa na Mratibu wa timu, Abbas Ally kutokana na mlinda mlango Aishi kuwa kambini kujiandaa na mchezo wa kesho wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Horoya.

Aishi amedaka asilimia kubwa ya mechi zetu pamoja na timu ya Taifa kwa mwaka mzima huku akiwa kwenye ubora mkubwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER