Mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Azam FC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.
Azam walipata bao la mapema dakika ya kwanza tu kupitia kwa Prince Dube baada ya kumalizia pasi ya James Akaminko.
Baada ya bao hilo tulitulia na kumiliki sehemu kubwa kipindi chote cha kwanza huku Azam wakirudi nyuma kuzuia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza kupitia pembeni kwa winga Kipre Jr.
Dakika ya 90 mlinzi wa kati Abdallah Kheri alijifunga na kutusawazishia bao hilo kwa kichwa wakati akifanya jitihada za kuokoa mpira uliopigwa na Kibu Denis.
X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Kennedy, Henock, Kanoute, Sakho (Kyombo 62) Mzamiru, Bocco (Baleke 57), Saido (Kibu 88), Chama.
Walionyeshwa kadi: Kennedy 15′ Kanoute 27′ Kapombe 35′
X1: Idrisu, Lusajo, Chilambo, Amoah, Kheri, Ndala, Bajana (Zayd 78), Akaminko, Dube, Sopu (Lyanga 62) Kipre (Idd Nado).
Walionyeshwa kadi: Dube 29′ Amoah 41′ Akaminko 45′