Kikosi chetu leo asubuhi kimefanyiwa vipimo vya Covid-19 ili kutambua hali zao za kiafya kuhusu ugonjwa huo ikiwa ni sehemu ya kuchukua tahadhari.
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeweka utaratibu wa kabla ya mchezo wowote lazima kufanyike vipimo vya Covid-19 ili kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo ambao ulitikisa dunia.
Hata hivyo, hakuna cha kuhofia kwa kuwa hakuna yeyote miongoni mwetu kwenye msafara wetu ambaye ameonyesha dalili za ugonjwa huo lakini kwa kuwa ni takwa la kikanuni kutoka CAF hivyo lazima tufanye.
Majibu ya vipimo hivyo yatatolewa saa 12 baada ya zoezi kukamilika na yatawekwa hadharani.