Mohamed Mussa ni Mnyama

Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Mohamed Mussa kutoka Malindi ya Zanzibar.

Mussa ambaye mbali na kucheza kama mshambuliaji pia anamudu kucheza kama kiungo wa nafasi zote za pembeni amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu yetu.

Miongoni mwa sifa ambazo zimetufanya kuvutiwa na kumsajili mchezaji huyo ni kipaji chake halisi cha mpira pamoja umri wake wa miaka 22, tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwa siku za usoni.

Ingawa anatokea Visiwani Zanzibar hii haitakuwa mara ya kwanza kushiriki Ligi Kuu ya NBC amewahi kuzitumikia timu za Gwambina FC na Mbeya City.

Usajili wa Mussa unakuwa ni wa nne katika dirisha hili dogo baada ya Saido Ntibazonkiza, Hamed Ismael Sawadogo na Jean Baleke na rasmi hapo tumefunga usajili kwa wakati huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER