Queens, Yanga Princess hakuna mbabe

 

Timu yetu ya Simba Queens imetoka sare ya bao moja na watani wetu Yanga Princess katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukifika zaidi langoni mwa Yanga katika dakika 15 za kwanza lakini tulikosa umakini wa kutumia nafasi tulizotengeneza.

Princess walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Chioma Wogu dakika za nyongeza kipindi cha kwanza kwa kichwa akimalizia mpira wa kona.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuongeza mashambulizi langoni mwa Yanga ambao walikuwa nyuma muda mwingi.

Vivian Corazone alitusawazishia bao hilo dakika ya 58 baada ya kupiga mpira mrefu wa moja kwa moja kufuatia mlinda mlango wa Yanga kutoka.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Pambani Kuzoya, Koku Kipanga, Joelle Bukuru na kuwaingiza Asha Djafar, Vivian Corazone na Olaiya Barakat.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER