Kikosi chetu kimewasili salama mchana huu mkoani Kagera tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Jumatano saa moja usiku katika Uwanja wa Kaitaba.
Kikosi kimetokea jijini Mwanza baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Geita Gold jana katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Timu imeondoka kikosi kizima cha wachezaji 24 ambao tuliosafiri nao kutoka jijini Dar es Salaam kamili kwa ajili ya mchezo wa Jumatano.
Baada ya kuwasili wachezaji watapata muda wa kupumzika kidogo na baadae watafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kujiweka sawa.
Kesho saa moja usiku kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Kaitaba kabla ya kushuka dimbani keshokutwa Jumatano.