Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa CCM Kirumba tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold utakaopigwa saa 10 jioni.
Wachezaji wote 24 wameshiriki mazoezi hayo na jambo la kushukuru hakuna yeyote ambaye amepata maumivu yatakayomfanya kukosa mchezo huo.
Tutaingia katika mchezo wa kesho tukiwaheshimu Geita lakini tumejiandaa kuhakikisha tunavuna alama zote tatu ugenini.