Mgunda Kocha Bora NBCPL Novemba

Kocha wetu Juma Mgunda amechaguliwa Kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC kwa mwezi Novemba.

Mgunda amewashinda Hans Van Pluijm wa Singida Big Stars na Meck Mexime wa Kagera Sugar ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Novemba Mgunda ametuongoza kushinda mechi nne na kutoka sare mbili kati ya sita tulizocheza.

Mechi nne tulizoshinda ni dhidi ya Ihefu, Namungo, Ruvu Shooting na Polisi Tanzania na tukitoka sare dhidi ya Mbeya City na Singida Big Stars.

Hii ni mara ya kwanza kwa Mgunda kushindika tuzo ya kocha bora wa mwezi tangu ajiunge na kikosi chetu Septemba mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER