Nahodha Opa Clement amechaguliwa mchezaji bora wa mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Green Buffaloes tulioibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Opa amekuwa na mchango mkubwa kwenye mchezo huo ambao umetupa tiketi ya kutinga nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika ikiwa ni timu ya kwanza Afrika Mashariki kufika hatua hiyo.
Opa alitupatia bao la pili dakika ya 79 baada ya kumalizia pasi ndefu kutoka kwa mlinzi wa kati Daniela Kanyanya kutoka nyuma.
Opa anakuwa mchezaji wa pili kutoka kikosini kwetu kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mechi baada ya Pambani Kuzoya kufanya hivyo katika mchezo uliopita dhidi ya Determine Girls.