Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeweka hadharani ratiba ya Ligi ya Mabingwa upande wa Wanawake ambayo itaanza Oktoba 30 nchini Morocco.
Timu yetu ya Simba Queens ambayo inawakilisha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati itafungua dimba kwa kuwakabili wenyeji AS FAR kutoka Morocco mchezo utakaopigwa Oktoba 30.
Baada ya mchezo huo Queens itapata siku mbili za kufanya mazoezi kabla ya kushuka dimbani kuikabili Determine Girls ya Libya, Novemba 2.
Queens itacheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Novemba 5 kwa kuikabili Green Buffalos kutoka Zambia.
Michuano hiyo inajumuisha timu nane zilizopangwa katika makundi mawili ambapo kila kundi litatoa timu mbili zitakazofuzu hatua ya nusu fainali.