Alichokisema Bocco kuelekea mchezo dhidi ya De Agosto

Nahodha wa timu John Bocco, amesema licha ya kuwa na historia nzuri kwenye Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, haitupi kiburi kuwa tutaibuka na ushindi kirahisi ugenini dhidi ya Premiero De Agosto Jumapili badala yake tutapambana mwanzo mwisho.

Bocco amesema kila mchezo una maandalizi yake na jambo zuri ni kuwa kikosi chetu kimejaa wachezaji wenye uzoefu wa michuano hiyo hivyo haitakuwa changamoto kwetu kucheza ugenini.

Bocco ameongeza kuwa tunakwenda Angola tukiwa tunajua wapinzani wetu De Agosto watakuwa na faida ya kuwa na mashabiki wengi uwanjani kuwaongezea morali lakini tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri.

“Maandalizi yamekamilika, walimu wetu wamejitahidi kutuelekeza kitu ambacho tunapaswa kwenda kukifanya nasi wachezaji tupo tayari kukitekeleza uwanjani. Tumewasoma wapinzani wetu na tunajua pia nao wametusoma hivyo tunajuana.

“Haitakuwa mechi rahisi ukizingatia kila timu iliyofika nafasi hii huwezi kuibeza, tutacheza kwa tahadhari zote ili mchezo wetu wa marudiano nyumbani tuwe kwenye mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya makundi,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER