Timu yafanya mazoezi ya mwisho Mo Arena

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaofanyika katika dimba la Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Morali ya wachezaji ipo juu na wote wamefanya mazoezi tayari kwa mchezo huo ambao tumeupa kipaumbele kuhakikisha tunashinda na kubaki na alama zote tatu nyumbani.

Wachezaji watatu Shomari Kapombe na Peter Banda ambao ni majeruhi wao hawajafanya mazoezi kutokana na kuendelea kupata matibabu wakati Pape Sakho amepata msiba.

Lengo letu ni kuhakikisha tunapambana kushinda mchezo wa kesho ili kurejea tena kileleni mwa msimamo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER