Nyota wetu Clatous Chama na Henock Inonga ambao walikuwa kwenye majukumu ya timu za taifa wamerejea nchini tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigiwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Chama alikuwa na kikosi cha Timu ya Taifa ya Zambia ‘Chipolopolo’ wakati Henock alikuwa na DRC katika mechi za kirafiki za kimataifa zilizopo kwenye kalenda ya FIFA.
Wawili hao wanaungana na wenzao ambao wameingia kambini jana kutoka Visiwani Zanzibar tulipokuwa na kambi ya wiki moja ambapo tulicheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Malindi SC na Kipanga FC.
Nyota wengine waliokuwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kilichokwenda Libya, Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mzamiru Yassin na Habib Kyombo nao wamejiunga na wenzao kambini.
Viingilio vya mchezo wa Jumapili vitakuwa kama ifuatavyo:
Mzunguko Sh 5,000
VIP B na C Sh 10,000
VIP A Sh 15,000