Mchezo dhidi ya De Agosto kupigwa Oktoba 9, Angola

Mchezo wetu wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CD Primeiro De Agosto utapigwa Oktoba 9, mwaka huu katika Uwanja wa Novemba 11 mjini Luanda, Angola.

Uwanja wa Novemba 11 ni miongoni mwa viwanja vikubwa nchini Angola na una uwezo wa kuingiza mashabiki 50,000.

Mchezo wetu wa marudiano utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Oktoba 16.

Kama kawaida malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote mbili ili kufuzu hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Tumetinga hatua hii baada ya kuitoa Nyasa Big Bullets kutoka Malawi kwa jumla ya mabao 4-0 kwenye michezo yote miwili tuliyocheza nao.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER