Mgunda amtaja Matola ushindi dhidi ya Big Bullets

Kocha mkuu wa muda Juma Mgunda, amesema amekikuta kikosi kikiwa kwenye hali nzuri chini ya Kocha Msaidizi Seleman Matola na ndiyo siri ya ushindi wa mabao 2-0 tuliopata dhidi ya Nyasa Big Bullets leo.

Mgunda amesema baada ya kupewa jukumu hilo alikaa na Matola kujua hali ya wachezaji ilivyo ili kuibadili kwa muda mfupi kitu ambacho kimesaidia kupatikana kwa ushindi huo.

Mgunda ameongeza kuwa baada ya kuongea na Matola ilibidi akutane na wachezaji wenyewe ambao ndiyo watekelezaji wa mbinu uwanjani kitu ambacho kimesaidia kupatikana kwa ushindi.

Pamoja na mtaji huo wa mabao mawili ugenini Mgunda amesema hatuwezi kujiona kama tumefuzu tayari kwakuwa kuna dakika 90 nyingine wiki ijayo jijini Dar es Salaam.

“Tumeshinda ugenini ni jambo jema lakini bado hatujafuzu tuna dakika 90 nyingine za nyumbani ambazo tunahitaji kufanya vizuri ili kujihakikishia nafasi nzuri,” amesema Mgunda.

Mchezo wa leo ni wa kwanza kwa Mgunda kuisimamia timu tangu apewe majukumu ya kocha mkuu wa muda siku nne zilizopita.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER