Mangungu aongoza Wanasimba kumuaga Dk. Gembe

Mwenyekiti wa Klabu Upande wa Wanachama, Murtaza Mangungu amewaongoza wanachama, wapenzi na mashabiki kuaga mwili wa aliyekuwa daktari wa timu yetu Yassin Gembe aliyefariki dunia Septemba 2, mwaka huu.

Mangungu ameongozana na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi na wachezaji nyumabani kwa marehemu Mbweni kabla ya kusafirishwa kuelekra Korogwe, Tanga kwa mazishi.

Baada ya kudumu kama daktari wa timu wa klabu yetu kwa takribani miaka 10 Gembe alipewa majukumu mengine ya kuwa daktari wa timu ya vijana nafasi aliyodumu nayo mpaka anakutwa na mauti.

Mwili wa marehemu Dk. Gembe utazikwa kesho Jumatatu nyumbani kwao Manundu, mjini Korogwe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER