Queens iko tayari kwa Fainali ya CECAFA kesho

Kocha Mkuu wa Simba Queens, Sebastian Nkoma amesema kikosi chake kiko tayari kwa ajili ya mchezo wa Fainali ya Michuano ya CECAFA dhidi ya SHE Corporates ya Uganda utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex saa moja usiku.

Nkoma amesema lengo la kwanza ni kuhakikisha tunashinda na kuchukua ubingwa kuwapa furaha mashabiki wetu na kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nkoma ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na anaamini SHE Corporates watakuja kivingine hasa baada ya kuwafunga katika mchezo wa hatua ya makundi.

“Kikosi kipo tayari morali kwa wachezaji ipo juu, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili kuchukua ubingwa,” amesema Nkoma.

Kwa upande wake mshambuliaji Aisha Juma amesema wao kama wachezaji wapo kamili ingawa wanafahamu mchezo utakuwa mgumu lakini lengo ni moja kuchukua ubingwa.

Naye kiungo fundi Joelle Bukuru, amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kutupa sapoti huku akiwaahidi kuwapa furaha.

“Sisi tupo tayari tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kushinda kikubwa tunahitaji mashabiki waje kwa wingi uwanjani kutupa sapoti,” amesema Joelle.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER