Wachezaji wapewa mapumziko ya siku tatu

Baada ya ligi kusimama kupisha mechi za kufuzu Fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) katika ya Tanzania na Uganda wachezaji wamepewa mapumziko ya siku ya tatu.

Wachezaji walifanya mazoezi ya utimamu wa mwili jana (recovery) baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar na baadae wakapewa mapumziko.

Wale walioitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wameruhusiwa kujiunga na wenzao na watarejea baada ya kumaliza majukumu hayo.

Baada ya mapumziko hayo wachezaji watarejea mazoezini kujiandaa na mechi zinazofuata ambapo tunatarajia kupata michezo kadhaa ya kirafiki.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER