Queens yatinga Nusu Fainali CECAFA

Kikosi chetu cha Simba Queens kimetinga Nusu Fainali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) baada ya kuifunga Yei Joints Stars ya Sudan Kusini mabao 4-0.

Kiungo mkabaji Vivian Corazone alitupatia bao la kwanza dakika ya 13 baada ya kumalizia mpira wa kona uliopigwa na nahodha Fetty Densa.

Wakiwa bado wanajishauri Yei Joints tuliwafunga bao la pili dakika ya 21 kupita kwa Philomena Abakah aliyepokea pasi ya Diana William.

Nyota Opa Clement alitupatia bao la tatu dakika ya 30 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Aisha Juma na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ambapo dakika ya 64 Philomena tena alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne.

Matokeo haya yanatufanya kushinda kwa asilimia 100 katika mechi za hatua ya makundi huku tukifunga mabao 11 na kutoruhusu bao lolote.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER