Baada ya kusubiri kwa muda mrefu hatimaye leo tumezindua jezi mpya ambazo tutazitumia katika mashindano yote ndani ya Msimu wa Ligi 2022/23.
Jezi zetu zipo kwenye ubora mkubwa kuanzia zilivyotengenezwa kimwonekano
Jezi zilizozinduliwa ziko aina tatu kama kawaida yaani ya nyumbani (nyekundu), ugenini (nyeupe) na jezi namba tatu (kijivu).
Baada ya uzinduzi huu wa jezi zitaanza kuuzwa katika maduka yote ya Vunjabei nchi nzima ambapo Wanasimba wataenda kununua kwa ajili ya mtoko husani wa kesho kwenye Tamasha letu la Simba Day.
Tunawaomba Wanasimba kununua jezi kwa wingi ili kesho kwenye Tamasha letu pale Benjamin Mkapa tupendeze kama kawaida yetu.