Mzamiru asaini mkataba mpya

Klabu yetu imefikia makubaliano ya kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili kiungo mkabaji, Mzamiru Yassin.

Mzamiru ni miongoni mwa mihili mikubwa ya kikosi chetu na kiwango chake hakijawahi kutetereka tangu tumsajili kutoka Mtibwa Sugar miaka sita iliyopita.

Uongozi baada ya kupitia ripoti ya mwalimu umeridhishwa na kiwango cha Mzamiru na kumuongezea kandarasi mpya.

Kuelekea msimu mpya wa ligi 2022/23 tunaendelea kuimarisha kikosi ikiwemo kuwaongezea mikataba wachezaji ambao tunaamini bado ni msaada mkubwa kwetu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER