Kikosi chetu kimeanza mazoezi jioni ya leo nchini Misri tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2022/23 chini ya kocha mkuu Zoran Maki.
Kikosi kimewasili alfajiri Misri katika mji wa Ismailia ambapo tunafanya mazoezi katika Hoteli ya Mercure Ismailia Forsan Island
Timu imesafiri na wachezaji 19 ambapo tunatarajia wataongezeka baada ya kukamilika taratibu za safari
Kikosi kitakuwa hapa kwa takribani wiki tatu ambapo tunaamini tutakapo rejea nyumbani tutakuwa tayari kwa msimu mpya.