Timu yafanya mazoezi Magazan

Kikosi chetu kimeendelea na mazoezi katika Uwanja wa Magazan kujiandaa na mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane utakaopigwa keshokutwa Jumamosi.

Wachezaji wote 24 tuliosafiri nao wameshiriki mazoezi hayo na morali zao zipo juu kuelekea mchezo huo ambao tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Mazoezi hayo yamefanyika katika uwanja huo kwa siku ya pili ambapo baada ya hapo saa tisa mchana kitaanza safari ya kuelekea katika mji wa Oujda ambao kutapigwa mchezo wenyewe.

Baada ya kufika Oujda kikosi kitafanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Manispaa ya Berkane ambao utatumika kwa mchezo wetu siku ya Jumamosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER