Mukwala apiga hat trick tukiichakaza Coastal Sheikh Amri Abeid

Mshambuliaji Steven Mukwala amefunga hat trick katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Hat trick hii ambayo ni ya kwanza kwake msimu huu imemfanya Mukwala kufikisha mabao nane kwenye ligi mpaka sasa.

Mukwala alitupatia bao la kwanza dakika ya 30 kwa shuti kali la chini chini baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na David Kameta ‘Duchu’.

Mukwala alitupatia bao la pili dakika ya pili ya nyongeza kipindi cha kwanza baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu.

Mukwala alitupatia bao la tatu dakika ya 57 baada ya kumalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango Chuma Ramadhani kufuatia shuti kali lililopigwa na Mpanzu.

Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 21 tukiwa nafasi ya pili huku tukiwa na mchezo mmoja mkononi.

X1: Chuma, Aidan, Miraji, Lawi, Viva, Semfuko, Sabri (Bagayoko 78′) Gustavo (Nkosi 85′) Maabad, Kikoti (Msimu 62′) Maulid (Mbaraka 63′)

Waliionyeshwa kadi: Kikoti 36′ Aidan 40′

X1: Ally, Duchu, Nouma, Chamou, Hamza, Kagoma (Ngoma 63′), Kibu (Mutale 77′), Fernandez, Mukwala (Ateba 77′), Ahoua (Awesu 58′), Mpanzu (Chasambi 77′)

Waliionyeshwa kadi: Chamou 43′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER