Kikosi chetu leo saa 10 jioniĀ kitashuka katika Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo ulioko Mbweni kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Kocha Abdelhak Benchikha amefanya mabadiliko ya wachezaji watatu ukilinganisha na kikosi kilichoanza dhidi ya Geita Gold.
Benchikha amewaanzisha Ayoub Lakred, Babacar Sarr na Said Ntibazonkiza kuchukua nafasi za Aishi Manula, Mzamiru Yassin na Pa Omar Jobe.
Hiki hapa kikosi kamili kilivyopangwa:
Ayoub Lakred (40), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Kennedy Juma (26), Che Malone (20), Babacar Sarr (33), Said Ntibazonkiza (10), Sadio Kanoute (8), Kibu Denis (38), Fabrice Ngoma (6), Clatous Chama (17).
Wachezaji wa Akiba
Aishi Manula (28), David Kameta (3), Israel Mwenda (5), Hussein Kazi (16), Edwin Balua (37), Mzamiru Yassin (19), Luis Miquissone (11), Freddy Koubalan (18), Pa Omar Jobe (2)