Tunaitaka ‘Hasa’ Mechi ya Marudiano ya Al Ahli Tripoli

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema tumeuchukulia kwa umuhimu mkubwa mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahli Tripoli utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ahmed amesema kwa kuona umuhimu huo Uongozi wa klabu umeamua kushusha viingilio ili kuwapa nafasi Wanasimba kujitokeza kwa wingi na kuujaza Uwanja.

Ahmed amongeza kuwa katika mchezo huo hatuangalii faida ya kupata pesa nyingi za viingilio bali tunawahitaji Wanasimba wengi ili kuwamaliza Al Ahli Tripoli.

“Kiingilio cha Shilingi 3000 tulikiacha toka zamani lakini tumekirejesha tena kwenye mchezo wa Jumapili ili watu wengi waweze kujitokeza.

“Hebu fikiria kama Mwanasimba kama titashindwa kufuzu hatua ya makundi kwenye michuano hii tena tukiwa nyumbani ni fedheha kiasi gani utajisikia mtaani, kwahiyo hilo halitakiwi kujitokeza tena,” amesema Ahmed.

Hivi hapa Viingilio vilivyotangazwa:

Mzunguko – 3,000
Orange – 5000
VIP C – 10,000
VIp B – 20,000
VIp A – 40,000

Tiketi zinaendelea kuuzwa kwa njia ya mtandao na vituo pia vimetangazwa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER