Tumepata ushindi dhidi El Qanah

Mchezo wetu wa kirafiki dhidi ya El Qanah FC inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri uliopigwa katika Uwanja wa Canal Suez umemalizika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mchezo huo ulichezwa kwa vipindi vitatu vya dakika 40 kila kimoja ili kuwapa nafasi ya kucheza wachezaji wote.

Kiungo mshambuliaji Jean Charles Ahoua alitupatia bao la kwanza dakika ya 14 baada ya kupiga mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja.

Ahoua tena alitupatia bao la pili dakika mbili baadae baadae baada ya walinzi wa El Qanah kushindwa kuzuia pasi iliyopigwa na mlinzi Karaboue Chamou.

Katika dakika 40 za pili kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko kuwatoa Ally Salim, Jean Ahoua, Freddy Michael Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Malone, Karaboue Chamou, Fabrice Ngoma, Joshua Mutale na Edwin Balua.

Na kuwaingiza Hussein Abel, Kelvin Kijili, Valentine Nouma, David Kameta, Saleh Karabaka, Debora Fernandes na Ladaki Chasambi, Augustine Okajepha na Valentino Mashaka.

Katika dakika 40 za tatu kocha Fadlu alifanya mabadiliko ya kuwatoa Debora, Kijili na Mashaka na kuwaingiza Awesu Awesu, Steven Mukwala na Abdulrazack Hamza.

Okejepha alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la tatu dakika ya 40 baada ya kupokea pasi safi ya chini chini kutokea kwa Chasambi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER