Simba yatwaa taji la VPL kwa kutoa dozi ya 4G

Timu yetu imekabidhiwa taji la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kuifunga Namungo FC mabao 4-0 katika mchezo wa mwisho wa msimu uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Medie Kagere alitupatia bao la kwanza dakika ya 18 kwa shuti la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi ya Chris Mugalu.

Mugalu alitupatia bao la pili dakika ya 25 baada ya kumalizia mpira uliopigwa na Shomari Kapombe kutoka upande wa kulia.

Mugalu aliongeza bao la tatu dakika ya 66 baada kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Kapombe kufuatia Luis Miquissone kuanzisha kwa haraka mpira wa adhabu.

Nahodha John Bocco alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne kwa mkwaju wa penati dakika ya mwisho baada ya kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Rally Bwalya, Ibrahim Ame na Clatous Chama na kuwaingiza Bocco, Kennedy Juma na Hassan Dilunga.

Ushindi kwenye mchezo huu unatufanya kumaliza msimu wa ligi 2020/21 kwa pointi 83 baada ya kucheza mechi 34.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER