Queens yaanza kwa kupoteza SLWPL

Kikosi chetu cha Simba Queens kimepoteza mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Wanawake Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) kwa mabao 2-1 dhidi ya JKT Queens.

Mchezo ulikuwa mzuri huku timu zikishambuliana kwa zamu lakini mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja ambapo tulimiliki kwa kiasi kikubwa.

Nahodha Opa Clement alitupatia bao letu kwa mkwaju wa penati dakika ya 23 baada ya Pambani Kuzoya kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

JKT walisawazisha bao hilo dakika ya 33 kabla ya kuongeza la ushindi kabla ya kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi tukiliandama lango la JKT ambapo dakika ya 80 kiungo mkabaji Vivian Corazone alikosa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa maafande hao kuunawa mpira ndani ya 18.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Esther Mayala, Vivian na Asha Djafar na kuwaingiza Olaiya Barakat, Jackline Albert na Amina Mohamed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER